Huku taifa likijiandaa kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya waathiriwa wa ajali, almashauri ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA imeendelea kuwahamasisha madereva wa magari ya uchukuzi wa umma kuwa waangalifu barabarani.

NTSA kwa ushirikiano na wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma imeandaa zoezi la kuchunguza afya ya macho ya madereva ili kuimarisha usalama wao na abiria barabarani. Kulingana msimamizi wa NTSA katika bonde la ufa Joseph Gichohi amesema kuwa hatua hii itasaidia kupunguza ajali barabarani.

Hafla ya kuadhimisha siku hiyo itaandaliwa tarehe 20 mwezi huu ambapo taasisi mbalimbali ikiwemo baraza la vyombo vya habari nchini MCK, limejitokeza na kuwahimiza madereva kufuata sheria za barabarani ili kuzuia maafa.

Kulingana na data za NTSA, Kenya ilirekodi vifo 4,579 kutokana na ajali za barabarani mnamo mwaka wa 2021,huku maelfu ya watu wakijeruhiwa vibaya. Kufikia tarehe 22 Mei 2022, vifo 1,816 zaidi vilirekodiwa, ikionyesha ongezeko la zaidi ya 9% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka wa 2021.

November 17, 2022