Ezekiel Machogu

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesisitiza utayari wa serikali katika kuifanikisha mitihani ya kitaifa inayotarajiwa kuanza baadae mwezi huu.

Akizungumza katika Kaunti ya Kisumu alipokutana na Wakuu wa shule na wakurugenzi wa elimu katika kaunti hiyo, Waziri machogu alitoa hakikisho kuwa uadilifu wa mitihani ya mwaka huu sio jambo la kutiliwa shaka na yeyote.

Waziri huyo pia ameweka peupe kuwa wizara ya elimu imefanikisha zoezi la kutoa masanduku yapatayo 493 ya kuiweka mitihani katika maeneo yote ya taifa.

November 17, 2022