BY ISAYA BURUGU 9TH MARCH,2023-Waziri wa elimu Ezekiel Machogu hivi leo amefika mbele ya kamati ya elimu ya Seneti kuzungumzia mstakabali wa elimu nchini.

Waziri ametakiwa kutoa mwanga Zaidi kuhusu   Elimu ya sekondari msingi na sekondari kwa ujumla baada ya  washika dau kwenye sekta ya elimu na wazazi kuibua maswali kuhusu utekelezaji wa mtaala mpya wa CBC sawa na  hali ya elimu kwa wanafunzi wa grade ia saba.

Waziri akizungumza mbele ya kikao hicho ameguzia maswala mengi kwenye sekta ya elimu yakiwemo mwongozo wakiusalama kwenye shule za mabweni, na kuwashughulikia wanafuzni walio na mahitaji maalum.

 

 

 

March 9, 2023