Gavana wa Narok Patrick Ntutu amezindua shehena ya pili ya dawa ambayo itasambazwa kwa hospitali na zahanati mbalimbali katika kaunti ya Narok. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika hospitali ya rufaa ya Narok Ntutu  amedokeza kuwa serikali yake inapania kuimarisha huduma za matibabu kwa kuanzisha mpango wa kutoa dawa za bure kwa wakaazi wa Narok.

Aidha gavana huyo amewaonya wafanyakazi wa hospitali wanaochukua dawa bila idhini hali inayochangia uhaba wa dawa katika hospitali hiyo ya rufaa na hospitali zinginezo kaunti ya Narok. Kufikia sasa serikali ya Narok imetoa jumla ya dawa milioni 92.

October 26, 2022