Radio Osotua › Local News

Mamlaka ya mawasiliano yafuta leseni za utangazaji za World Evangelism na Times TV.

Local News April 28, 2023 John Waicua

Mamlaka ya mawasiliano nchini imefuta leseni za vituo viwili vya Runinga vinavyohusiana na wahubiri Paul Makenzi na Ezekiel Odero, kwa kigezo cha kukiuka mwongozo wa leseni za utangazaji.

Katika notisi iliyochapishwa na mwenyekiti wa mamlaka hiyo Ezra Chiloba siku ya Ijumaa, leseni za utangazaji za  vituo vya World Evangelism na Times TV zimefutwa mara moja kwa kukiuka Zaidi ya kanuni 12 na 17 mtawalia za utangazaji. Katika notisi hiyo aidha,kampuni inayopeperusha picha kwa niaba ya vituo hivyo imeombwa kusitisha upeperushaji huo mara moja.

Wahubiri hao wawili wanaendelea kuchunguzwa wakihusishwa na vifo katika eneo la Shakahola.