MP. John Kiarie

Wabunge katika bunge la kitaifa wamekubaliana kwa kauli moja kuiidhinisha hoja ya mbunge wa Dagoretti John Kiarie, itakayowalazimu wanakandarasi kuipanda miti iliyong’olewa wakati wa ujenzi wa barabara.

Hoja hii ambayo sasa inasubiri hatua za mwisho ili kuwa sheri, pia imeitaka serikali kuweka kipengee cha upandaji wa miti katika mipango yote ya ujenzi wa barabara.

Hoja hii imejikita katika kifungu cha 42 cha Katiba – kinachosema kwamba kila mtu ana haki ya kuwa na mazingira safi na yenye afya na pia katika Ibara ya 69(1)(d) inayoiagiza Serikali kushirikisha umma katika usimamizi, ulinzi na uhifadhi wa mazingira.

November 17, 2022