Marais wastaafu Olusegun Obasanjo na Uhuru Kenyatta wameongoza mazungumzo ya amani kati ya maafisa wa serikali ya ethiopia na wawakilishi wa kundi la wapiganaji wa Tigray jijini Nairobi. Viongozi hao wawili wameelezea matumaini kuwa mazungumzo hayo yatarejesha utulivu na amani ya kudumu nchini Ethiopia.

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa kumekuwa na mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa TPLF eneo la Tigray nchni Ethiopia hali ambayo imepelekea maafa huku maelfu ya watu wakilazimika kuhama makwao na wengine wakikabiliwa na baa la njaa.

November 7, 2022