Rais Wiliam Ruto ameondoka nchini leo kuelekea nchini Ethiopia ambapo amepangiwa kukutana na Waziri mkuu wa taifa hilo Abiy Ahmed Ali.Viongozi hao wawili watakuwa na mazungumzo ya Pamoja kuhusu kuboresha uchumui na mazingira ya kuendesha biashara kati ya nchi hizi mbili.Baadaye wataongoza kuzinduliwa kwa huduma za  simu za kampuni ya Safaricom.Ruto amesindikizwa katika uwanja wa ndege wa JKIA na naibu rais Rigathi Gachagua ,Waziri Mteule  wa maswala ya kigeni Alfred Mutua,mbunge wa Garisa mjini Eden Duale kati ya wengine.

 

 

 

 

October 6, 2022