Mwanafunzi wa kiume wa chuo kikuu cha Maasai Mara  Narok ameaga dunia baada ya kuzama ndani ya mto Narok alipokuwa akiogelea pamoja na wenzake jana jioni. Kulingana na taarifa za polisi Mwanafunzi huyo kutoka kaunti ya Nyamira alikuwa katika mwaka wake wa kwanza na alikuwa anasomea maswala ya Siasa ya Sayansi (political science) katika chuo hicho.

Maafisa wa polisi walipata taarifa kuhusu mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 26 kuzama kutoka kwa wanafunzi wenzake waliokuwa wakiogelea pamoja naye kwenye mto huo wa Narok eneo la Seventy nine estate.

Maafisa wa polisi walifika pale na kuanza kutafuta mwili huo ambapo walifanikiwa kuupata na wakaupeleka hadi hifadhi ya maiti katika hospitali ya rufaa ya Narok huku upasuaji ukitarajiwa kufanywa.Visa vya wanafunzi kutoka chuo hicho kuzama ndani ya mto huo wakiwa wanaogelea vimekuwa vikishuhudiwa mara kwa mara.

October 31, 2022