Naibu Rais Rigathi Gachagua amezindua mpango kabambe wa ujasirimali kwa ushirikiano na sekta ya kibinafsi unaolenga kubuni angalau nafasi za kazi milioni moja katika mwaka ujao. Mpango huo kwa jina la Kenya Youth Employment and Entrepreneurship Accelerator Programme (K-YEEAP), umezinduliwa jijini Nairobi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Gachagua amepongeza jumuiya ya wafanyabiashara kwa kushirikiana na serikali inapotafuta suluhu la tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini. Rigathi ameongeza kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana nchini unakadiriwa kuwa 38.9% huku takriban vijana 800,000 wakiingia katika soko la ajira kila mwaka kutoka kwa taasisi za elimu ya juu. 

Naye kwa upande waziri wa michezo na masuala ya vijana Ababu Namwamba ameahidi kufanya kazi kwa karibu na sekta hiyo ya kibinafsi ili kubuni nafasi zaidi za ajira kwa vijana. 

October 31, 2022