Naibu Rais Rigathi Gachagua ameirai idara ya mahakama nchini kuangazia mabadiliko katika mfumo wa hukumu, na kuanzisha hukumu zitakazosaidia katika uhifadhi wa mazingira badala ya kifungo cha nje.
Gachagua aliyekuwa akizungumza katika siku ya mwisho ya kongamano la idara ya mahakama barani Afrika lililokuwa likiangazia jukumu la mahakama katika kulinda mazingira, alisema wengi wa wanaopatikana na hatia za kufanya makosa madogo, huenda wakaosa kuwa na uwezo wa kulipa faini wanazotozwa mahakamani, hivyo hukumu za kupewa majukumu ya kuyatunza mazingira zitawafaa zaidi.
Gachagua alieleza kwamba hatua hii itakua njia mojawapo ya njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia idara ya mahakama, na pia kuimarisha mfumo wa haki nchini.
https://twitter.com/rigathi/status/1643597705678143490?s=20