Rais William Ruto amewaonya wafanyakazi wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA dhidi ya kuendeleza ufisadi.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasilisha rekodi yake ya ulipaji ushuru katika makao makuu ya KRA, rais Ruto alisema kuwa kuna baadhi ya maafisa wa KRA wanaoshirikiana na watu wanaokwepa kulipa ushuru suala ambalo anasema limeathiri pakubwa pato la taifa.

Vilevile aliwahimiza wasimamizi wa KRA kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inapata sura mpya iwapo inapania kuafikia malengo yake katika ukusanyaji ushuru.

Share the love
May 26, 2023

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

%d bloggers like this: