ALL SAINTS DAY

By John Msafiri

Watakatifu ni nani ?

Ni watu waliomtumikia Mungu kwa uaminifu mkubwa hapa duniani,na ambao Mungu anawatunza kwa furaha huko mbinguni.

Ushuhuda wao haukuwa wa maneno matupu bali kwa kumwaga damu yao,ndiyo kutoa maisha yao.
Kanisa limeendelea kuamini kwanza kuna mamilioni ya watakatifu wasiofahamika na watu,bali kwa Mungu mwenyewe.

Kwa kuwa idadi yao ni kubwa na ni vigumu kuwatendea haki kwa kila mmoja wao ,ndiyo maana kanisa likaamua tangu mwaka 800 Ad kuadhimisha sherehe ya pamoja ya watakatifu wote.
Hatimaye kabisa lilipitisha kila tarehe 1 November iwe ni sherehe kwa ajili ya watakatifu wote kwa kanisa katoliki kote ulimwenguni.

Watakatifu waliishi kama sisi hapa duniani wakakombolewa kwa upendo na uwezo wa Mungu na Sasa wanafurahia heri ya uzima pamoja na Mungu na Malaika.

Tulipakwa mafuta wakati wa ubatizo kwa ishara ya Msalaba,kila tuonapo au tufanyapo ishara hiyo,tunakiri kuwa sisi ni mali ya Mungu.

Wanatuambia tuendelee na mapambano kwa nia ya kushindana pasipo kushindwa.Tena wanaahidi kutusaidia kwa sala zao kwa Mungu baba yetu.

Sisi wakristo ni kweli ni watoto wa Mungu
( 1Yn 1:3 -1 ).
Kwa ubatizo tumeanza kushiriki maisha ya kiroho.
Tunaye Roho yule yule wa Bwana wetu Yesu Kristo,ni Roho huyo huyo anayeendelea kutufanya kuwa Watakatifu.

Kutoka 39:30
“Nao wakafanya hilo pambo la hiyo taji takatifu la dhahabu safi,na kuandika juu yake andiko mfano wa kuchorwa kwa muhuri,“MTAKATIFU WA BWANA.”

Tunaambiwa kuwa makuhani wakuu wa Israel walivaa pambo-Taji Takatifu,
lililochorwa mithili ya muhuri, “MTAKATIFU WA BWANA au waliowekwa wakfu kwa Bwana”
Tulipakwa mafuta wakati wa ubatizo kwa ishara ya Msalaba,kila tuonapo au tufanyapo ishara hiyo,tunakiri kuwa sisi ni mali ya Mungu.

Yohani katika kitabu cha ufunuo anatueleza jinsi alivyoona katika ndoto umati mkubwa wa watu waliovaa mavazi meupe wakibeba matawi ya mitende mikononi mwao Kama alama ya ushindi.
Mzee wa umri akamweleza Yohane,
“Hao ndiyo wale wanaotoka katika ile dhiki kuu,nao wamefua mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya mwanakondoo” Ufunuo 7:14.

MATESO,TAABU,USUMBUFU AU UGUMU WA MAISHA VITUTIE NGUVU YA KUBAKI WAAMINIFU KWA KRISTO.

November 1, 2022