Kinara wa Muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga ameshtumu kitendo cha kuteketezwa kwa kanisa na msikiti katika eneo la Kibra jioni ya jana. Odinga ameelekeza kidole cha lawama kwa naibu wa Rais Rigathi Gachagua kwa kitendo hicho anachosema kilinuia kuzua mgogoro kati ya wajanamii wa eneo hilo.
Odinga aliyasema haya alasiri ya leo katika kikao na waandishi wa habari, akieleza kwamba wanaohusika katika upangaji wa vurugu wanafahamika waziwazi.
Wakati huo huo Raila ametaka mataifa ya nje na marafiki wa kigeni kuvunja kimya chao na kuzungumzia yale yanayoendelea nchini. Pia ameahidi kwamba jitihada za kutafuta haki zinazoongozwa na mrengo wa upinzani hazitakoma kwa vyovyote vile.
Raila Odinga kwa mara nyingine amelaani uvamizi ulioshuhudiwa hapo jana katika kampuni yake na ardhi ya familia ya Kenyatta, huku akiwalaumu maafisa wa polisi kwa kuwarushia vitoa machozi waandamanaji licha ya wao kuandamana kwa njia amani kama ilivyo kwenye katiba.
https://twitter.com/RailaOdinga/status/1640736347588534272?s=20