Katika jamii yoyote ile humu nchini, kulikua na mfumo maalum, uliotumiwa kama ishara kwamba mwanajamii amevuka katika daraja la utu uzima na kuacha kufanya mambo ya kitoto.

Katika jamii ya Abagusii, daraja hili lilitiwa chapa kwa kupitia tohara iliyotekelezwa kwa wanajamii wote wa kiume kati ya miaka 10 hadi 14. Baada ya kuvunja ungo na kuanza kubaleghe, mvulana katika jamii hii alianza kutuma ujumbe kwa wazee kwamba amefikisha umri wa kupashwa tohara, wazee hawa walidadisi ujumbe huu, kisha kuamua iwapo mvulana huyu amehitimu kupelekwa jandoni au la.

Katika makao haya mapya, Moto mkubwa uliwashwa, moto ambao haukufaa kuzimika hadi watakapotoka na kuanza kutagusana tena na wanajamii. Wasimamizi waliokuwa na jukumu la kuwatunza pia walikuwa na jukumu la kuutunza moto huu kwani kulikuwa na madhara ambayo yangetokea iwapo  ungezimika.

Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke

May 26, 2023

Leave a Comment