Katika jamii ya Abagusii, mwongozo wa tamaduni ulielekeza kwamba wazazi walikua na jukumu la kumtafuta mchumba kwa mwana wao. Wazazi wa mvulana hivyo basi walianza jukumu hili punde tu walipohisi kwamba mwana wao amefikia umri wa kuoa. Kwa mujibu wa mmoja wa waelekezi wetu katika makala haya mzee Amenya Minchira, wazazi wa mvulana na msichana huyu walitumia ishara na mazungumzo yasiyo ya wazi ili kuweza kuwakutanisha wawili hawa.

Baada ya kufikisha ujumbe huu na kupokelewa vizuri, mchakato wa kuelekea akikatika boma la msichana ulianza mara moja, mzee huyu mwenye mvulana akiandamana na wazee wenzake pamoja na wavulana wengine ili kuanza makubaliano kuhusu wawili hawa na jinsi ya kulipa mahari.

Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke

June 20, 2023

Leave a Comment