Rais William Ruto amezidua mradi wa ujenzi wa Nyumba za bei nafuu eneo la Starehe katika kaunti ya Nairobi kutwa ya leo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo ambao ni mradi wa tano wa aina hii baada ya kuongoza miradi sawia katika maeneo ya Homa Bay, Ruiru, Kibera na Shauri Moyo, Rais amesema kwamba nyumba zinazojengwa zitakuwa za wakenya wa kiwango cha chini, akitoa haikikisho kwamba watakaohusika katika ujenzi wa nyumba hizi watakuwa wenyeji wa maeneo ya Starehe na maeneo jirani.

Aidha rais ameeleza kwamba wanakandarasi watakaosimamia ujenzi wa nyumba hizi, watawashusisha wafanyakazi wa kike kwa kiwango sawia na wale wa kiume, akipongeza mchango wa kinadada katika miradi ya aina hii.

Kiongozi wa taifa aliandamana na viongozi wengine serikalini, wnaaojumuisha Naibu wake Rigathi Gachagua, Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja pamoja na wawakilishiwadi kutoka maeneo husika.

March 6, 2023