Rais Ruto Turkana

Rais William Ruto ameongoza msururu wa mipango ya Serikali ya kitaifa ya kutoa chakula cha msaada kuzisaidia familia zilizoadhirika na uhaba wa chakula kufuatia kiangazi kinachoshuhudiwa katika sehemu mbali mbali nchini.

Rais Ruto ambaye aliwaongoza viongozi wa kaunti ya Turkana katika kuwapa wananchi chakula katika eneo hilo amesema kwamba serikali italazimika kutafuta shilingi billion 10 zaidi ili kukabiliana ipasavyo na ukosefu wa chakula.

Akizungumza katika hafla sawia katika kaunti ya Samburu, Rais ameahidi kuwa shughuli hii itatekelezwa kila mwezi hata maeneo mengine kama vile shuleni na hospitalini.

November 5, 2022