Radio Osotua › Local News

Rais Ruto amteua Caleb kositany kama mwenyekiti wa halmashauri ya viwanja vya ndege nchini

Local News March 17, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU,17TH MARCH,2023-Rais William Ruto amemteua aliyekuwa mbunge wa Soy  Caleb Kositany kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya bodi ya mamlaka ya viwanja ya ndege nhini.

Kositany, ambaye ni rafiki wa karibu wa rais  Ruto, atashikilia wadhifa huo kwa muda wa miaka mitatu kwa mjibu wa notisi katika gazeti rasmi la kiserikali  ya hivi leo Machi 17.

Vilevile mwingine aliye kwenye mkondo huo huo wa uteuzi na rais ni Wiliam Kimathi ambaye amechaguliwa  kama mwenyekiti wa  bodi ya huduma za kisheria  yakitaiafa kwa muda wa miaka sita ijayo.