Radio Osotua › Local News

Rais Ruto azindua shehena ya Oksijeni kueleka katika hospitali mbalimbali nchini.

Local News April 17, 2023 John Waicua

Rais William Ruto ameongoza zoezi la kuzindua shehena ya mitungi ya gesi ya Oxygeni, itakayopelekwa katika hospitali mbalimbali za kaunti kote nchini.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa katika ikulu ya Nairobi na kuhudhuriwa na magavana mbalimbali Pamoja na washirika wengine wa serikali katika sekta ya afya, rais ameeleza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kuimarisha huduma za afya nchini, na kusisitiza umuhimu wa serikali kupiga jeki upatikanaji wa huduma za afya zenye kiwango cha juu humu nchini.