Rais William Ruto amekariri kuwa atajikita kwenye katiba na sheria za taifa katika utendakazi wake, akieleza kwamba kutekeleza jambo lolote nje ya katiba kutalielekeza taifa katika njia isiyofaa.

Akizungumza baada ya kuongoza hafla ya kuapishwa kwa wakili mkuu Shadrack Mose katika ikulu ya Nairobi adhuhuri ya leo, Rais alisema kwamba ni muhimu kuhakikisha kuwa haki za kila mkenya zinazngatiwa, pasi na kuhitilafiana na haki za wananchi wengine. Pia alieleza Imani yake kwamba wakili mkuu Shadrack atatekeleza majukumu yake ipasavyo, kwa kutoa mwongozo unaohitajika wa kisheria kwa serikali katika kutekeleza majukumu yake.

Aidha Rais alimtaka Mose kuhakikisha kwamba sheria ya thuluthi mbili ya jinsia inatekelezwa ili kutoa fursa sawa kwa wanawake kushiriki katika uongozi wa nchi.

Moses anachukua nafasi ya Kennedy Ogeto aliyehudumu chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.

https://twitter.com/WilliamsRuto/status/1637802906400219137?s=20

March 20, 2023