Rais William Ruto amemteua Muyumba Simmon Indimuli kuwa Katibu wa Bodi ya Kamati ya Ushauri ya Mashirika ya Serikali kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Januari 30, 2023.

Mkuu wa Nchi, pia amemteua Ugas Mohamed kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji kwa kipindi cha miaka mitatu huku uteuzi wa Nick Nesbitt ukibatilishwa.

Sylvanus Maritim naye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano kwa muda wa miaka mitatu.

Waziri wa usalama wa ndani Prof. Kithure Kindiki kwa upande mwingine amewateua Ali Swaleh Nyamai, Ann Njeri Mathu, Mbunge wa zamani wa Emgwen Elijah Lagat, Fredrick Ngugi na Lucia Nzoongo kuwa wajumbe wa Bodi ya Kampeni ya Kitaifa ya Kupambana matumizi ya Dawa za Kulevya kwa kipindi cha miaka mitatu.

Aidha uteuzi wa John K. Cheruiyot, Alice Wanjira Mutuma na Dkt George Ogalo kwenye bodi hiyo umebatilishwa.

February 25, 2023