Mke wa rais wa Marekani Bi. Jill Biden amewasili nchini kwa ziara ya siku tatu na kupokoelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA, na balozi wa Marekani nchini Kenya, Pamoja na Bi. Rachel Ruto miongoni mwa viongozi wengine.

Ndege iliyombeba Bi Biden ilitua JKIA mwendo wa saa kumi unusu. Kiongozi huyo anatarajiwa kuangazia maswala ya haki za kina mama, na pia maswala ya watoto Pamoja na mikakati ya kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula ambalo limegubika mataifa mengi barani Afrika.

February 24, 2023