Zoezi la kuwapiga msasa mawaziri wateule lakamilika hii leo.

Zoezi la kuwapiga msasa mawaziri wateule limekamilika hii leo huku aliyekuwa waziri wa leba Simon Chelugui akiwa wa kwanza kuhojiwa. Chelugui ambaye ameteuliwa kama waziri wa vyama vya ushirika amerejelea maneno ya rais William Ruto na kueleza kuwa hustler fund haitakuwa ya…

Rais William Ruto aongoza maadhimisho ya 59 ya siku ya mashujaa.

Rais William Ruto ameongoza maadhimisho ya 59 ya siku ya mashujaa katika bustani la Uhuru jijini Nairobi hii leo.Hii ni sherehe ya kwanza ya kitaifa kuongozwa na rais Ruto tangu alipoapishwa kama rais wa tano wa taifa hili.Ruto ameahidi kufanya kazi na…

Zoezi la kuwahoji mawaziri wateule laendelea kwa siku ya tatu bungeni.

Zoezi la kuwahoji mawaziri wateule limeendelea kwa siku ya tatu,seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen akiwa wa kwanza kufika mbele ya kamati inayoendesha zoezi hilo. Murkomen ambaye ameteuliwa kama waziri wa barabara na uchukuzi amesema kuwa miradi mingi ya barabara imesitishwa kutokana…

Madereva waliosafirisha vifaa vya kupigia kuwa waandamana kudai malipo yao mwezi mmoja baada ya uchaguzi mkuu.

Madereva waliosambaza vifaa vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa agosti tisa huko Transmara wameandamana katika makao makuu ya IEBC mjini Kilgoris wakidai malipo yao. Maafisa wa IEBC eneo hilo walitoroka na kufunga afisi zao kutokana na kizaazaa hicho. Wakizungumza na waandishi…