Rais William Ruto amezindua rasmi hazina ya hustler fund ambapo wakenya sasa wataweza kupata mikopo kuanzia shilingi mia tano hadi shilingi elfu hamsini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika katika stesheni ya magari ya greenpark, rais Ruto amesema kuwa fedha hizo zitawasaidia wakenya wenye mapato ya chini na ambao walikuwa wamepigwa marufuku kuchukua mikopo Zaidi.

Naye kwa upande wake naibu rais Rigathi Gachagua ametoa wito kwa wakenya ambao watachukua mkopo huo kuulipa kwa wakati unaofaa ili kuhakikisha kuwa mpango huu hausitishwi

Wakenya ambao wangependa kuchukua mkopo huo, wanahitajika kujisajili kupitia nambari *245#.

November 30, 2022