BY ISAYA BURUGU 8TH MAY 2023-Waziri wa usalama wa ndani na ushirikishi wa serikali kuu Prof Kindiki Kithure hivi leo ametembelea gereza la Mwea katika kaunti ya Kirinyaga kukagua mageuzi yanayoendelea kutekelezwa kwenye gereza hilo yakiwemo matumizi yam ashine na vifaa vya kisasa kwenye mashamba za magereza nchini.

Waziri akizungumza kwenye gereza hilo amesema kuwa serikali itato shilingi bilioni moja kwa kila gereza katika muda wa miezi michache ijayo zitakazotumiwa katika kuendeleza mageuzi hayo.

Ameongeza kuwa serikali imo mbioni kuwasilisha vifaa haswa vitanda na magodoro yakutosha kuhakikisha kuwa kila mfungwa analalia kitanda chake na kufurahia mazingira wanamoishi

.

Vilevile ametangaza  kuwa jopo lililobuniwa kutathmini jinsi ya kufanya mageuzi kwenye idara ya polisi a magereza linaloongozwa naye aliyekuwa jaji mkuu David Maranga hivi karibuni litawasilisha ripoti yake ya mwisho kwa rais .

 

 

 

 

 

May 8, 2023