Ripoti ya utenda kazi wa mahakama nchini sawa  na utekelezaji  wa haki iliyozinduliwa leo imebainisha kuwa upungufu wa wafanyakazi wa idara hiyo ndio kikwazo kikuu katika utekelezaji jukumu lake. Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyoandaliwa katika majengo ya mahakama ya juu, rais William Ruto amesema kuwa serikali imejitolea kuboresha mgao wa bajeti kwa mahakama kila mwaka ili kusaidia katika utoaji wa haki kutoka chini kwenda juu kwa kuongeza idadi ya Mahakama za makosa madogo, kuanzisha vituo vya Mahakama Kuu pamoja na kusaidia mpango wa kidijitali wa mahakama. Ruto vilevile ameitaka idara ya mahakama kuwafuatilia na kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaokwepa kulipa ushuru.

Naye kwa upande wake Naibu wa rais Rigathi Gachagua, ameipongeza mahakama kwa kutupilia mbali mswada wa marekebisho ya katiba BBI uliopendekezwa na aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta pamoja na kinara wa azimio la umoja-one kenya Raila Odinga.

November 4, 2022