BY ISAYA BURUGU 1ST SEPT,2023-Serikali inalenga wakulima 176000 katika wamu ya pili ya usajili wa ruzuku ya mbolea katika kaunti ya Migori.

Kamishna wa kaunti ya Migori David Gitonga aliyekuwa akizungumza katika mkutano uliyowaleta Pamoja wakuu wa kilimo kutoka serikali ya kaunti,utawala wa mkoa na polisi ,amesema kuwa serikali itaka kuhakikisha kuwa inafikiwa asilimia mia kw amia ya wakulima wanolengwa.

Gitonga anasema wkaulima wanaweza kupata mbolea hiyo ya ruzuku iwapo watasajiliwa.

Kamishna huyo wa kaunti amesema kuwa wakulima ambao walisajiliwa kwenye awamu ya kwanza lakini hawakupata mbolea hiyo wanafaa kutumia fursa hiyo kusahihisha maelezo.

 

 

 

 

 

 

 

Share the love
September 1, 2023