Wabunge kutoka eneo la magharibi wamekutana na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi ambapo wameahidi kufanya kazi pamoja kwa maendeleo ya eneo hilo.

Wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa muungano wa wabunge wa Kanda ya Magharibi John Waluke walikutana na Mudavadi katika kikao cha kiamsha kinywa na kueleza kujitolea kwao kwa umoja wa eneo hilo.

Kando na hayo wameisisitiza haja ya kuungana na kutetea maslahi ya eneo hilo.Mkutano huo ulikuwa wa kwanza wa aina yake baada ya kipindi cha uchaguzi.

Viongozi hao waliazimia kufanya kazi pamoja na kushauriana katika masuala ya manufaa kwa eneo hilo chini ya uongozi wa Mudavadi na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula.

November 23, 2022