Serikali imepunguza bajeti ya jumla ya mwaka huu wa kifedha kwa KSh132.46 bilioni kutoka KSh3.981 trilioni hadi KSh3.848 trilioni.

Hili ni punguzo la asilimia 3.3. Tangazo hili lilitolewa wakati Rais William Ruto alipotia saini kuwa sheria Mswada wa bajeti ya ziada wa 2024 na Mswada wa ugavi wa mapato wa 2024 katika Ikulu ya Nairobi.

Kwa mujibu wa rais Ruto ni kwamba miswada hiyo itahakikisha kuwa miradi ya kufufua uchumi itapata pesa za kutosha sawa na kuimarisha utoaji wa huduma za serikali.

June 10, 2024