Ulimwengu ukiadhimisha siku ya usalama wa deta, serikali imewahakikishia wakenya kuwa data kuwahusu iko salama.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha siku hii, rais William Ruto amesema kuwa serikali itahakikisha kuwa wahalifu hawatumii teknolojia kukwepa kulipa ushuru au kuwalaghai wakenya wenzao.

Aidha rais Ruto ameitaka wizara ya teknolojia kuhakikisha wakenya wamewezeshwa kujitambulisha kidijitali. Ruto vilevile ameahidi kuisaidia Ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa data kupata uwezo unaohitajika ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

January 27, 2023