Waziri wa elimu Ezekiel Mcahogu amezindua nakala mpya za gredi ya saba huku wanafunzi wa gredi ya sita wakitarajiwa kujiunga na gredi hiyo au junior secondary tarehe 30 mwezi huu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ulioandaliwa katika makao makuu ya KICD, Machogu amesema kuwa usambazaji wa nakala hizo ambao umeigharimu serikali shilingi bilioni 3 umejiri baada ya wizara ya elimu kufanya tathmini katika shule mbalimbali ili kufahamu utayari wao kwa wanafunzi wa junior secondary. Usambazaji huo utakamilika wiki ijayo.

Machogu ameeleza kuwa Kila mwanafunzi wa gredi ya 7 katika shule za umma atapewa nakala ya masomo yote na kuweka wazi kuwa wamezindua nakala 17,893,270 za wanafunzi na nakala 423,514 za mwongozo wa mwalimu.

Hali kadhalika waziri huyo amedokeza kuwa wizara ya Elimu imeendelea kusambaza vitabu vya CBC kwa wanafunzi kulingana na sera yake ya kila mwanafunzi anastahili kupata kitabu kimoja ili kuhakikisha ufundishaji bora.

Aidha amewahimiza wazazi ambao wanao watajiunga na gredi ya 7 kuhakikisha kwamba watoto wao wanaripoti shuleni siku ya Jumatatu.

January 27, 2023