Katibu Mkuu wa Huduma za Matibabu kwenye wizara ya afya Harry Kimtai, alizindua rasmi Ripoti ya Makadirio ya Akaunti ya wizara ya Afya ya Kitaifa kwa mwaka kifedha 2019/20 hadi 2021/22.

Ripoti hiyo inasisitiza dhamira ya serikali ya upatikanaji wa huduma za afya kwa usawa na inaangazia maendeleo makubwa chini ya mpango wa ruwaza ya 2030, ikiwa ni pamoja na matibabu ya bure ya maradhi kama vile ukimwi, malaria na kifua kikuu, ambayo yamepunguza kwa viwango vikubwa vifo vya watoto na kina mama wajawazito.

Aidha katibu Kimtai alitambua changamoto zinazoendelea kuikumba sekta ya afya kama vile upatikanaji wa matibabu usio na usawa, uhaba wa fedha, na uhaba wa wafanyakazi wa afya wenye ujuzi.

Alisisitiza umuhimu wa kuendelea na juhudi za kukabiliana na magonjwa ya kuambukizana na yasiyo ya kuambukizana. Ripoti hiyo ya Hesabu za Kitaifa za Afya vilevile itasaidia katika kukusanya rasilimali na uundaji wa sera unaozingatia ushahidi.

May 22, 2024