Issa Timamy

Gavana wa kaunti ya Lamu Isa Timamy, sasa ndiye kinara mpya wa chama cha Amani National Congress almaarufu ANC baada ya kukabidhiwa mikoba ya kuongoza chama hicho mapema leo na mkuu wa mawaziri humu nchini Musalia Mudavadi.

Mudavadi alijiondoka kutoka katika usimamizi wa chama hicho, baada ya uteuzi wake kuingia katika baraza la mawaziri. Katika taarifa yake muda mfupi baada ya kuidhinishwa rasmi, gavana huyo Pamoja na viongozi wengie wa chama cha ANC wamekubali kushirikiana na kuahidi kukiimaricha chama chao kueleka katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Viongozi wa chama cha ANC pia wameahidi kuandaa kikao cha kuangazia sababu za chama cha ANC kuandikisha matokeo ya kukata nyono katika uchaguzi mkuu uliokamilika mwezi Agosti mwaka huu.

November 15, 2022