Makamishna wa IEBC

Vikao vya kusikilizwa kwa malalamishi dhidi ya makamishna wanne wa IEBC na jopo linaloongozwa na jaji wa mahakama ya rufaa Aggrey Muchelule vimeng’oa nanga hii leo.

Wakili wa kamishna Irene Masit, Donald Kipkorir amepinga kuanza kwa vikao hivyo akidai kuwa kesi hiyo inahusisha ushahidi mpya wa hatikiapo ambao haukutolewa katika kamati ya bunge kuhusu sheria wakati malalamishi dhidi ya makamishna hao yalipoangaziwa.

Kufikia sasa ni kamishna mmoja tu ambaye hajajiuzulu kutoka kwa tume hiyo. Waliojiuzulu ni pamoja na naibu mwenyekiti Juliana Cherera, Francis Wanderi na Justus Nyang’aya.

December 20, 2022