Kikao maalum cha kujadili hoja ya kubanduliwa kwa gavana wa Meru Kawira Mwangaza kinaendelea hivi sasa katika bunge la seneti.

Maseneta wamelazimika kukatiza likizo yao ili kuhudhuria kikao hicho baada ya wawakilishi wadi wa Meru kumbandua mamlakani gavana huyo kwa madai ya utumizi mbaya wa ofisi na kukiuka sheria.

Hoja ya kubanduliwa kwa Mwangaza ilipendekezwa kwa mara ya kwanza na mwakilishi wadi wa Abogeta magharibi Dennis Kiogora  tarehe 22 mwezi Novemba.

Aidha magavana kupitia baraza la magavana nchini, walijitokeza hiyo jana kusimama na Mwangaza, wakiwaomba maseneta kujikita katika sheria kabla ya kufanya maamuzi ya kumwondoa mamlakani gavana huyo.

December 20, 2022