Wakaazi wa eneo la Amhara nchini Ethiopia ambalo lilichukuliwa tena na wanajeshi wa serikali hivi karibuni wamewashutumu wapiganaji kutoka eneo la Tigray kwa unyanyasaji ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela.

Wilaya ya Raya Kobo ilishikiliwa kwa wiki tano na vikosi vya Tigray. Wakazi hao wamedai kwamba watu wanaoshukiwa kuwa wanaviunga mkono vikosi vya serikali walilengwa.

Pande zote za mzozo kaskazini mwa Ethiopia hapo awali zimeshutumiwa kwa kukiuka haki za kimataifa za binadamu.Uchunguzi wa pamoja uliofanywa mwaka jana na Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia (EHRC) na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ulisema kunaweza pia kuwa na ushahidi wa uhalifu wa kivita.

Unyongaji usio wa kimahakama, utesaji, ubakaji, na mashambulizi dhidi ya wakimbizi. Hata hivyo,vikosi hivyo vimekanusha madai hayo mara kadhaa.

 

October 12, 2022