Radio Osotua › Local News

Wakaazi wa Narok watakiwa kutumia fursa ya sasa ambapo mvua inashuhudiwa kupanda mashamba yao

Local News March 16, 2023 Osotua

 BY ISAYA BURUGU,16TH MARCH,2023-Waakazi wa kaunti ya Narok wametakiwa kuchukua fursa ya mvua inayoshuhudiwa kwa sasa katika sehemu bali mbali katika kaunti hii kutayarisha mashamba yao na kupanda.

Wito huu umetolewa na kaunti kamishna anayeondoka Isaac Msinde.

Masinde amewataka wakulima hao kufika kwenye maeneo watakayoagizwa kuchukua mbolea inayotolewa na serikali ili kuwawezesha kufanikiwa katika msimu wa upanzi.Kaunti ya Narok imeanza kushudia mvua baada ya kiangazi cha muda mrefu.