Taifa la Kenya limeungana na ulimwengu mzima hii leo, katika kuiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake, inayotoa nafasi ya kuyasherehekea mafanikio ya wanawake pasi na kuwabagua kwa misingi ya kikabila, kitamaduni, kiuchumi au kisiasa.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu, ilikuwa Kukumbatia usawa, iliyokuwa ikitoa rai kwa walimwengu kuanza gumzo kuhusu upatikanaji wa nafasi sawa kati ya wanawake na wanaume. Makundi mbalimbali ya kutetea maslahi ya wanawake yalikongamana kwa maadhimisho ya siku hii kwa njia mbali mbali, huku viongozi mbalimbali wakitoa rai zao kuhusu siku hii.

Rais William Ruto katika ujumbe wake siku ya leo, alieleza kufurahia hatua kubwa ambazo taifa lipepia kuelekea katika kuafikia usawa wa kijinsia, akieleza utayari wa taifa kusonga mbele katika kufanikisha uswa Zaidi. Kinara wa Upinzani Raila Odinga, naye ametoa woto wa kuimarishwa kwa upatikanaji wa usawa, ili kuwasaidia kuvunja mipaka ya kitamaduni, kkijamii na hata kiuchumi.

Kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hivi leo, Mke wa Rais Bi. Rachel Ruto aliwatembelea wafungwa wanawake katika gereza la Langa’ta jijini Nairobi, huku akiwahimiza wanawake hao kujitoza kwenye sekta ya ubunifu ili wapate ujuzi utakaowasaidia wanapomaliza vifungo na kurejea nyumbani.

 

March 8, 2023