Himizo limetolewa kwa wanaosimamia miito kanisani kuwaelekeza vijana katika njia bora za kikristu, ili wawe vielelezo bora katika jamii kadhalika kupata mapadre wengi kwenye siku za usoni.

Akizungumza na idhaa hii baada ya kuwahutubia mapadre wa jimbo katoliki la Eldoret katika kituo cha kipastorali cha St John Paul, askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu la Nyeri Peter Kairo, amewataka wasimamizi wa miito katika parokia zote kuwaombea vijana na kuwaelekeza kwani ndio viongozi wa siku za usoni.

Kulingana na askofu huyo mkuu, wito hutoka kwa Mungu na vijana wanapaswa kushauriwa ili waitikie miito na kumtumikia Mwenyezi Mungu.

Wakati huo huo  askofu  kairo  amewahimiza mapdre kumtegemea Mwenyezi Mungu na kusali kila wakati ili kukuza imani yao kuwa dhabiti. Vilevile amewahimiza mapdre kujivunia wito wa kumtumikia Mungu na kumtumikia bila kukoma.

February 10, 2023