Watu kadhaa wamejeruhiwa na wengine kutekwa nyara katika shambulizi lililofanyika katika kituo cha treni nchini Nigeria.

Kulingana na polisi, watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwavamia abiria waliokuwa wakisubiri treni huku juhudi za kuwasaka waliotekwa nyara zikiendelea.

Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti kwamba karibu abiria 30 wametekwa nyara ila hakuna kundi lililodai kuhusika na uvamizi huo kufikia sasa.

Mnamo mwezi Machi mwaka 2022 wanamgambo wa Boko Haram waliwauwa kwa kuwapiga risasi watu 8 na kuwateka nyara wengine katika shambulizi lililofanyika katika kituo cha treni karibu na Mji Mkuu Abuja.

January 9, 2023