Washukiwa watano wanaojifanya kuwa maafisa wa Mamlaka ya Ushuru nchini wametiwa mbaroni mjini Narok wakiwatishia wafanyabiashara wa vileo.

Watano hao ni pamoja na afisa maarufu wa serikali. Maafisa walifanikiwa kupata stakabadhi muhimu kutoka kwa washukiwa ambazo zitatumika kama ushahidi dhidi yao.

Kwa mujibu wa Inspekta Davis Muindi Simiyu, ana jumla ya kesi tano zinazoendelea mahakamani kwa makosa ya kujifanya maafisa wa KRA, tatu katika Mahakama ya Nakuru na nyingine mbili katika Mahakama ya Milimani.

Washukiwa hao kwa sasa wanazuiliwa na polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka ya kujifanya kuwa maafisa wa KRA, kughushi stakabadhi na makosa mengine yanayohusiana nayo.

December 14, 2022