Rais William Ruto anapania kuangazia upya utendakazi wa idara ya polisi, ili kuiwezesha idara hii kutekeleza majukumu yao kwa ustaarabu, pasi na kukiuka haki za kibinaadam kwa wakenya wake.

Katika hotuba yake mchana wa leo, Rais Ruto ameahidi kubuniwa kwa jopokazi litakalohakiki na kuangazia upya utendakazi wa idara za usalama nchini, ili kuepuka mizozo kati ya raia na asasi za usalama, sawa na taarifa zinazowahusisha maafisa wa polisi na utekelezaji wa maovu humu nchini.

Katika kipindi cha kampeni kuelekea katika uchaguzi mkuu, viongozi wa Kenya Kwanza wakiongozwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua walitoa ahadi ya kutekeleza mageuzi mengi katika huduma ya polisi ili kuboresha huduma zinazotolewa katika idara hiyo.

Aidha Rais ameeleza kuwa baadhi ya mageuzi ambayo ametekeleza katika kipindi cha miezi 3 ya uongozi wake yameanza kuzaa matunda, akiwapongeza maafisa hao kwa juhudi zao za mchwa katika kulinda taifa.

 

December 12, 2022