Huku sikukuu ya krismasi ikijongea kwa mwendo wa kasi, serikali imeanzisha oparesheni ya kudhibiti uuzaji wa pombe haramu na ulanguzi wa dawa za kulevya kote nchini.

Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ushurikiano na serikali ya Kitaifa itaongoza zoezi hilo ambalo linalenga kuondoa pombe haramu na dawa za kulevya zilizopigwa marufuku mitaani huku ikiahidi kutohitilafiana na wafanyabiashara wa vileo wenye leseni halali.

Kulingana na katibu wa wizara ya mambo ya Ndani Dkt Raymond Omollo, oparesheni hii imeanzishwa kwa dhima kwamba baadhi ya wakenya huvutiwa na matumizi ya pombe haramu na mihadarati hasa msimu huu wa krismasi.

December 14, 2022