Idara ya Huduma za Polisi nchini (NPS) kwa ushirikiano na Maafisa wa Wanyamapori wa Kenya (KWS) wamefanikiwa kuwatia nguvuni washukiwa wawili waliokuwa na pembe mbili za ndovu katika Kaunti ya Embu.

Kulingana na taarifa kutoka NPS, washukiwa hao walikamatwa siku ya Ijumaa wakiwa na pembe tatu za tembo zenye uzani wa kilo 53, na zinadhaniwa kuwa nz thamani ya shilingi milioni 10.6.

Wawili hao sasa wanasubiri kufikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka ya umiliki wa pembe za ndovu, kosa ambalo linakabiliwa na adhabu kali kisheria.

September 23, 2023