Waziri wa Afya nchini Bi. Susan Nakhumicha kwa mara nyingine amesisitiza kujitolea kwa serikali katika kutoa msaada kwa serikali za kaunti ili kuziwezesha kutoa huduma za afya zenye kiwango kinachofaa.

Akizungumza katika kaunti ya Nyeri mchana wa leo alipomtembelea gavana wa kaunti hiyo Mutahi Kahiga, Waziri Nakhumicha alisema wizara yake itachukua jukumu la kuinua viwango vya huduma za matibabu zinazotolewa, na pia kuhakikisha kuwa wanawawezesha wananchi kupata huduma hizi kwa ukaribu zaidi.

Waziri wa afya amekua na msururu wa ziara katika kaunti mbalimbali, ambapo amekutana na viongozi wa kaunti hizi kwa nia ya kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya.

Kwa upande wake gavana Mutahi Kahiga ameeleza mpango wa kuinua baadhi ya hospitali katika kaunti hiyo, ili Kuhakikisha kuwa maeneno mbalimbali yananufaika na huduma hizi za afya. Gavana huyo ameeleza mpango wa kuhakikisha kuwa ndoto ya kuifikisha hospitali ya Mwai Kibaki hadi kiwango cha Level 6 inaafikiwa.

January 9, 2023