Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, amewataka machifu na manaibu wapo Pamoja na maafisa wengine wa uongozi wa mitaa, katika kaunti ya Murang’a kuimarisha vita dhidi ya pombe haramu na dawa za kulevya.

Akizungumza hii leo, Gachagua amesema kwamba visa vya uraibu wa pombe haramu na dawa za kulevya vimeongezeka maradufu katika kaunti hiyo na kaunti Jirani za maeneo ya mlima Kenya, akieleza kuwa machifu na maafisa wengine wamezembea katika utendakazi wao.

Aidha amewonya maafisa ambao pombe hiyo itaendelea kuuzwa katika maeneo yao kuwa watakabiliwa kisheria.Naibu wa rais alikua amehudhuria hafla ya kupeana fedha za masomo kwa wanafunzi wanaohitaji katika kaunti ya Murang’a, shughuli iliyoandaliwa katika uwanja wa Ihura.

January 26, 2023