Bunge la Kitaifa limemtaka waziri wa Kawi Davis Chirchir na Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya usambazaji umeme nchini Kenya Power Joseph Siror kufika mbele ya Kamati ya Bunge kuhusu Kawi Alhamisi wiki ijayo ili kujibu maswali kufuatia tatizo la kukatika kwa umeme kote nchini siku ya Ijumaa.

Kamati ya Kawi, inayoongozwa na Mbunge wa Mwala Vincent Musyoka, inawataka wawili hao kutoa maelezo ya kina kuhusu mambo yaliyosababisha hitilafu hiyo iliyoathiri maeneo mbalimbali ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA). Pamoja na kubainisha kuwa wawili hao ni lazima watoe maelezo ya kutosha kuhusu tukio hilo.

Kampuni ya Kenya Power ilithibitisha ripoti za kukatika kwa umeme kwa kiasi kikubwa katika taarifa yake siku ya Ijumaa ambapo ilihusisha kukatika kwa umeme huo na usumbufu wa mfumo mkuu.

Share the love
August 26, 2023