BY ISAYA BURUGU 2TH AUG 2023-Rais  William Ruto amewasili katika uwanja mdogo wa ndege wa kakamega jana jioni tayari kuanza ziara yake ya siku tano eneo la magharibi  inayoanza rasmi hivi leo.

Rais Ruto alipokelewa na mkuu wa mawaziri  Musalia Mudavadi, gavana wa Kakamega  Fernandes Barasa, Seneta  Boni Khalwale, miongoni mwa viongozi wengine  na maafisa wa serikali.

Kwa mjibu wa ratiba ya mipangilio yar ais kuhusu ziara hiyo,ataanza ziara yake  kwa kuzuru kaunti za Busia ana kakamega.Ambapo anatarajiwa kuzindua eneo la kutua kwa Samaki  la mukhuloba. huko Budalangi na baadaye kufungua hospitali ya rufaa ya kaunti mjini Busia

Kisha baadaye ,atasimama katika chuo kikuu cha Alupe eneo bunge la Teso kusini na kisha baadaye azindue muradi wa ujenzi wa nyumba za makaazi za gharama nafuu  huko Milimani katika eneo bunge la Lurambia.

 

August 26, 2023