BY ISAYA BURUGU,10TH MAY,2023-Zoezi la kutazama mwili wa hayati aliyekuwa mkewe mpiganiaji uhuru Dedan Kimathi Mukami Kimathi  litafanyika jumaosi hii kabla ya mazishi yake.

Mukami aliaga dunia  wiki jana akiwa na umri wa miaka 101.Katibu wa wizara ya usalama wa ndani Raymond Omollo, anayeongoza kamati ya mazishi anasema fursa ya kutazama mwili wake itafunguliwa  katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee jijini Nairobi kuanzia saa kumi na mbili za asubuhi hadi saa moja.

Kisha baadaye mwili huo utasafirishwa hadi nuyumbani kwake Njambini kaunti ya Nyandarua kwa mjibu wa mapenzi ya familia yake kwa mazishi.Viongozi  mbali mbali akiwemo kinara wa upinznai Raila Odinga  wameitaka serikali  kumzika Mukami  katika bustani ya Uhuru  kwa heshima ya wapiganiaji uhuru walioteswa hapo.

Wengine kama vile Waziri wa biashara Moses Kuria  walitaka mabaki ya mumewe  Kufukuliwa kutoka kaburi la Kamiti na kuandaliwa mazishi ya Pamoja  na mkewe Mukami nyumbani kwao.

 

 

 

 

May 10, 2023